Site Loader

CHUO KIKUU MZUMBEKITIVO CHA SAYANSI JAMII SOMO:                             FASIHIANDISHIPROGRAMU:                  BELM2MSIMBO WA KOZI:     KSW 200MHADHIRI:                    FULUGE,A.

AINA YA KAZI:              KAZIYA KUNDINAMBA YA KUNDI:      09WAHUSIKA   JINA NAMBA YA UDAHILI SAHIHI 1 CECILIA RODAFUNGO 15303050/T.16   2 ISAYA BATHOLOMEO 15303013/T.15   3 HARUNI M AMINI 15303003/T.16   4 JUBISI SAIDI 14304052/T.16   5 PETRO E EMMANUEL 15303060/T.16   6 SALMA ABDILLAH IDDY 15303029/T.16   7 SENKORO GABRIEL BARIKI 15303055/T.

Best services for writing your paper according to Trustpilot

Premium Partner
From $18.00 per page
4,8 / 5
4,80
Writers Experience
4,80
Delivery
4,90
Support
4,70
Price
Recommended Service
From $13.90 per page
4,6 / 5
4,70
Writers Experience
4,70
Delivery
4,60
Support
4,60
Price
From $20.00 per page
4,5 / 5
4,80
Writers Experience
4,50
Delivery
4,40
Support
4,10
Price
* All Partners were chosen among 50+ writing services by our Customer Satisfaction Team

16   8 TUMAINI ULOMI 15303014/T.16    SWALI:Falsafani imani na ukweli wa maisha ya mtu au watu katika jamii. Thibitisha madai hayakwa kubainisha vipengele vya Falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika kazi zawaandishi wafuataao;(i)                Mirathiya Hatari (C. Mng’ong’o)(ii)             BabuAlipofufuka (S.A. Mohamed)Falsafani dhana pana ambayo haina namna moja ya kuifasili, wataalamu mbalimbaliwametoa mawazo yao kuhusu dhana hii ya falsaafa. Miongoni mwao ni pamoja na;Wamitila (2003),anasema falsafa ni istilahi inayotumiwa kuelezea wazo au mawazo aliyo nayo mtuau mwandishi. Mfano falsafa ya mwandishi inaweza kulenga maisha, mila, desturi,au utamaduni wa jamii husika atokayo mwandishi.

TUKI (2004), wanasemafalsafa ni elimu ya asili, maana nasababu za maumbo au vitu au ni busara na hekima.Kwaujumla falsafa inaweza kufafanuliwa kuwa ni taaluma inayodadisi hali halisi yamaisha ya binadamu kwa kuzingatia Imani, mila, desturi pamoja na mienendoaliyonayo binadamu katika jamii yake huku akitafakari njia sahihi na bora zakuweza kutatua changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo katika maisha yake yakila siku.KuhusuFalsafa ya mwafrika wataalamu mbalimbali vilevile wameeleza maana yake.Wataalamu hao ni pamoja na, Placide Temples (1995), Oruka (1990) na Mbiti(2011) ambao wanaifafanua dhana hii kama “fikra au mitazamo wanayoishughulikiawaafrika wenyewe au watu wengine ambao wanakubali mila na desturi za kiafrika”.Wamitila (2003),anaeleza kwa kiasi kikubwa falsafa ya kiafrika inavyojidhihirisha katikahadithi.

Mfano hadithi ya Abunuasi. Hivyo tunaweza kusema kuwa falsafa yakiafrika ni dhana au mawazo ya waafrika wenyewe juu ya mambo mablimbaliwanayoyafanya kama vile imani juu ya maisha, mila, desturi, jinsi yakushirikiana katika jamii na kutafuta suluhisho juu ya matatizo au changamotozinazowakabili.Nikweli kabisa kwamba “Falsafa ni Imani na ukweli wa maisha ya mtu au watu katikajamii”. Kwa kutumia riwaya mbili ambazo ni MIRATHI YA HATARI iliyoandikwa na C.MNG’ONG’O (1977) na riwaya ya BABU ALIPOFUFUKA iliyoanddikwa na S. A MOHAMED(2001) tunathibitisha dai hili kwa kubainisha vipengele vya falsafa ya kiafrikavinavyojitokeza katika hizi kama ifuatavyo;Kwakuanza na riwaya ya MIRATHI YA HATARI iliyoandikwa na C.

MNG’ONG’O vipengelevya falsafa ya kiafrika vilivyojitokeza ni kama ifuatavyo;Falsafa ya imani katikasihiri na uchawi. Waafrika wanaamini kuhusu uwepo wa nguvuya sihiri na uchawi yaani huamini kuwa kila janga linalompata mtu lazima kunamkono wa mtu nyuma yake. Mfano magonjwa, kifo, ajali na kadhalika. Mwaandishiwa riwaya hii anathibitisha dai hili kwa kuonesha jinsi wananchi wa kijiji chaKilole huko Njombe wanapoamini uvaaji wa hirizi kwa ajili ya kujikinga nauchawi na uovu.

Mwandishi anamtumia mhusika Gusto ambaye ndiye amerithishwamirathi ya hatari kutoka kwa baba yake Kazembe mfano ukurasa wa (15-16) mzeeKazembe anamwambia Gusto “mwanangunakuachia kazi kubwa, ni urithi mkubwa ukiutumia vyema, bali pia ni mirathi yahatari usipojihadhali nayo. Nakuachia dawa zote za milki yangu katika mizunguya sihiri”. Pia uwepo wa kiapo cha uchawi unadhihirika pale ambapo Gustoanaapishwa kuwa ni uaminifu wa kuingia katika uchawi. Kiapo hicho kila mtuanahitaji ndipo awe mchawi. Mfano katika ukurasa wa (20_21), Gusto anaonekanaakiapa kwa kutamka maneno. Kiapo chenyewe kilikuwa hivi;                        “Nye msiha gya vakulu                         Nyevasehe yemwalonguwe                        Nye vayangu yetulilumwi                         Mpulih! Mpulihe nene                        Yenduhwi lapangila pahuta                         Sindilalonga! Sindilalonga,                        Nambi huhodza hela;                        Idza apa dza baha                        Wone ndilemwe ulu-hadatu!                        Ihipemb’ihi hinyanyage….!”Maanayake;                        “Enyi mahoka wa mababu,                        Enyi wazee mliotutangulia;                        Enyi wenzangu                         Sikilizeni kiapo changu!                        Sitasema wala kuwaza lolote,                         Landani ni landani                        Nishindwe mara tatu,                        Pembehili linichome moto…!”Falsafa ya uduara.

Katikawazo hili Temples anasema kuwa mwafrika hupenda vitu vya umbo la kiduara kwaniwanaamini kuwa hivyo ndivyo vitu vizuri ndo ndiyo mila na desturi zao.Mwandishi anadhihirisha hili pale Gusto anapomsifia mpenzi wake Dina kwa uzzurialio nao. Mfano katika ukurasa wa 30 Gusto anasema kuwa; “Dina alikuwa msichana wa kimo cha kawaida, mwenye ngozi ya maji yakunde, uso wake wa mviringo kidogo; uliopaambwa na jozi ya macho makubwa namaangavu na pua ndogo”. Dhana hii inajitokeza katika jamii zetu, mfanonyumba za msonge katika kanda ya ziwa, mikao ya kula huwa katika duara piavyombo vingi huwa katika umbo la duara kama vile sufuria, vyungu, ndoo, vinu,nyungo za kupepetea na ngoma. Falsafa ya uduara ina nafasi kubwa katika jamiikwani hudumisha na kuendeleza utamaduni wa mwafrika kwani tangu zamaniinaaminika kuwa kila kitu ni kizuri kikiwa katika umbo la udura.

Hofu ya uhai na kifo. Hiini hoja nyingine ya Temples kwani anaamini kuwa waafrika wanahofiauhai na kifo.Kwa kudhihirisha hili anangalia salamu zao wanapoagana kwa safari au mtuanapopatwa na ugonjwa anaamini huenda kifo kinamsogelea na huenda asipone. Wazohili linajitokeza katika riwaya hii pale Mzee Kazembe anapomweleza mwanae kuwahali yake ni mbaya na kifo kinamkaribia.

Haya yanajidhihirisha katika ukurasawa 15. Mzee Kazembe anasema; “siku zanguzimekwisha sidhani kama nitaishi Zaidi”. Pia mama yake Gusto anakuwa nahofu juu ya uhai wa Gusto na ndiyo maana anamhusia aachane na mirathialiyokabidhiwa na baba yake kwani anaweza akapoteza maisha. Haya yanadhihirikakatika ukurasa wa 38, mama yake Gusto anaposema;”Lakini nakuomba jambo moja,mwanangu, usijaribukucheza nao kwa madawa aliyokuachia baba yako.

Fahamu kuwawewe ungali mwanafunzi na wao ni mafundi! Watakuanuza bure mwanangu, sipendinimpoteze ten ahata mmoja wenu kabla sijafa”.Piasuala la salamuna kujua hali ya mtu inaonesha hofu ya kifo. Watu hujuliana halije, wanaendeleaje? Ama wamepatwa na umauti. Mfano katika riwaya hii Malipulaanapoenda nyumbani kwa kina Gusto wanaanza kujuliana hali (uk. 57), Gustoanaonekana akiwajulia hali Mzee Malipula na Mzee Kindimba; “habari za nyumbani wazee wangu?” “Nyumbani kwema tu, lakini hatujui yahuko nyuma” alijibu Mzee Kindimba. Hivyo basi falsafa ya uhai na kifo inanafasi kubwa katika jamii kwani inawafanya wanajamii kuchukua tahadhari ilikuzuia kifo. Pia inaendeleza Zaidi dhana ya kustawisha zaidi uhai.

Kwa upandemwingine falsafa hii ina hasara kwani hurudisha nyuma maendeleo kwasababu mtuataogopa kufanya jambo la maendeleo kwa kuhofia kifo ambacho kitamfanya kuachamali zote alizochuma pia kutotimiza malengo yake.Waafrika wanaamini katika suala landoa. Waafrika wanaamini sana katika ndoa zao na ndoa hizohudumishwa ili kupata watoto. Uhai wa binadamu unaanzia kwenye mimba ambayo nimatokeo ya ndoa. Wazo hili pia linaonekana katika riwaya hii. Mfano ndoa yamzee Kazembe (baba yake Gusto) na Nyamidze (mama yake Gusto), watoto nanewanapatikana na wanaokufa ni watano. Ukurasa wa 5 unaonesha hilo. Pia mjombawake Dina anakuwa na ndoa inayompelekea kupata watoto (Uk78).

Suala la ndoalinasawiri maisha halisi ya waafrika mfano kuna ndoa za kanisani, msikitini,serikali na za kijadi. Suala la ndo ndilo hupelekea kizazi cha kafrikakuendelea kwani wanaume huoa wanawake wengi na kuzaa watoto wengi zaidi ambaohuwa ndiyo nguvu kazi ya jamii na kuendeleza jamii zao. Vilevile mwafrikaanaamini uzazi ndiyo uzima wa milele na ugumba ni laana ambayo ni mbaya kulikozote. Hivyo fahari ya mwafrika ni kuwa na wake na watoto wengi kwa mantiki hiyofalsafa ya kiafrika inasema kuoa au kuolewa ni jambo la lazima bila kujali hataumri kwani kuna wazazi ambao wanawaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo auwanafunzi. Mfano katika riwaya ya takadini mhusika Shingai analazimishwa nawazazi wake kuolewa na Nhamo lakini Shingai anaonesha msimamo wake na kutorokanyumbani kwao na kwenda kulala na Takadini (uk.117).Mwafrika anatawaliwa sana na suala laukarimu na ushirikiano katika shida na raha. Temples anasemakuwa waafrika wamekuwa na ukarimu na ushirikiano hasa pale jirani ama nduguyake anapopatwa na tatizo kama vile msiba, ajali na mambo mengine yamfanyayo mtukuwa na huzuni.

Au kama kuna tukio la furaha kama vile kufanikiwa kitu Fulani,arusi, jando na unyago, sherehe za kuhitimu shule na sherehe zingine ambazozinamfanya mtu awe mwenye furaha. Katika mambo hayo yote waafrika wanakuwawakarimu pia hushirikiana ili kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa. Katikariwaya hii ya MIRATHI YA HATARI jambo hili linajidhihirisha hivi;”…msichanamdogo aliyekuwa anazungumza na mama”. “kamwene binti yangu habari ganizikuletazo asubuhi hii…” (uk.

49). “mimi nakwenda huko kwenye kilio labdanitarudi tu jioni kuchukua matandiko…” uk.50. Hivyokutokana na nukuu hiyo nidhahiri kuwa waafrika ni wakarimu na wanpendakushirikiana katika shida na raha na kwa hali na mali mfano kufanya kazikuchangiana na kadhalika.Miungu wengi.

Mwafrikaanaamini kuwepo kwa Mungu mkuu na miungu wengine wadogowadogo kama vile mizimuna mababu. Mwafrika anaamini kuwa kuna ngazi ama darajia tofautitofauti zakumfikia Mungu mkuu ambaye ndiyo nguvu kwa mizimu, wahenga (waliokufa), wazeewaliohai, binadamu wa kawaida. Dhana hii inajidhihirisha katika riwaya hii yaMIRATHI YA HATARI, ambapo Gusto ana nguvu za sihiri lakini bado anaamini kuwaMungu yupo. Anachukuliwa na madoda kwa ajili ya kuapishwa kuwa ndiye mrithi wacheo kile alichokuwa nacho baba yake lakini baadaa ya kuamka Jumapili badoanajiandaa kwenda kanisani. Mfano Gusto anasema; “…niliporudi niliingia chumbani, nikavaa nguo zangu rasmi tayari kwakwenda kanisani…” uk.

29. Hivyo hii inaonesha jinsi waafrika wanavyoaminiMungu, kuwa hata mambo yawe magumu au mepesi yeye pekee anaweza kuwafanikishamambo yao.Dhana ya wakati.

Kwawaafrika hawaangalii wakati na hawana haraka na wakati, mwafrika katikakuangalia wakati, namba za saa ni kitu dhahania, kwa mwafrika wakati hauamuimatendo kama ilivyo kwaa mzungu. Mfano katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI jambohili linajidhhirisha katika familiya ya mzee Kazembe alivyokuwa akijilimishausiku na mchana bila hata ya kuangalia wakati (uk.5). Pia mama yake Gusto(Nyamidze) anaonekana akifanya kazi bila kupumzika.

Mwandishi anasema; “Nyamidze yupi? Basi angeambiwa si Yule wamji wa Kazembe ajilimishaye usiku na mchana!” Hivyo hata katika jamii zetutunaona kwamba mwafrika hana ratiba wala mipaingilio mizuri ya kazi zao jambolinalotokea mbele yake hukabiliana nalo kwa wakati huo kwa mfano kukiwa na mvuaanaweza asifanye kazi yoyote au msiba ukitokea anakatisha shughuli zake bilakujali wakati. Hivyo kwa mwafrika wakati ni kitu halisi wala sio dhahania.Nakwa kutumia riwaya ya BABU ALIPOFUFUKA iliyoandikwa na SAID A MOHAMEDvifuatavyo ni vipengele vya falsafa vinavyojidhihirisha ndani yakeDhana ya familia pana. Mwafrikahuishi kwa kujitambulisha na familiya pana yenye kujumuisha waishio sasa,waliokufa na ambao hawajazaliwa. Kwa hiyo marehemu bado ni mtu kwa waafrika nafamiliya si baba, mama na watoto tu bali ni ukoo mzima.Katikariwaya hii mwandishi anaonesha jinsi familiya ya kina K ilivyo pana nainajumuisha watu walio hai na wali    okufakiasi kwamba wote hushirikiana kwa namna moja ama nyingine katika kuleta aukuondoa matatizo katika familiya.

Hii inadhihirika katika ukurasa wa 110 mwandishianasema; “kumbililikuwa kubwa ajabu. Lilikuwa tokea zamani limekusudiwa kuwa pahala pamapumziko ya koo za wenye jumba hilo la mabwana wakubwa na wake zao wannewannena vizazi vyao vilivyobarikiwa si haba”.Hivyofamiliya pana inadhihirika pale akina K wanaendelea kuwa na uhusiano na wazeewaliokufa, Maajuza, vijana na watoto wanaoishi katika jumba lililopo katikamtaa wa Kataa.Dini inavyozingatiwa. Kwamwafrika dini ni ya kuvumiliana. waafrika wanaheshima kwa wahenga, miunguwengi, kuna mawasiliano kati ya miungu na wahenga, kuna mawasiliano kati yamiungu/mizimu na watu wa kawaida kupitia wazee, maakuhani, miviga na matambiko.

Hivyo watu huomba na kupokea majibu ya shida zao kupitia hizo darajia au ngazikwani huzieshimu na kuzithamini. Kwa mfano katika riwaya hii mwandishianaonesha jinsi Mzuka anavyotoa heshima na kuongea na wahenga au mizimu uk.141.

“hapotena ndipo yule mzuka alipotimka mpaka pale penye mwili wa bahari. Akapiga kofikubwajuu yake na maji yakaruka kwa mpasuko mkubwa. Sasa akaikabili baharikusema nayo”. “Nauka …nauka… narudi mimi mjumbe wenu. Nimeshatekelezam’liyonituma.

Huyu hapa mtu wenu. Tumefika ukingoni. Nasema na nyinyimahakimuwakati … Nyinyi ms’omwanzo wala mwisho. Nyinyi wa zamani na wasasa. Mpokatika kutokuwepo.

Mnaokufa huku mkiishi. Nyinyi mnaoona yote. Mnaosikia yote.

Msioweza kukimbilika. Wenye kupiga na kuharibu na kupanga na kutengeneza wakatimmoja. Nyinyi sehemu ya mimi!” Hivyo ndivyo waafrikawamekuwa wakihusiana na miungu ama mizimu katika maisha yao kwani hutoa heshimana kuleta haja zao kwa miungu, wahenga ama mizimu kupitia wazee.Ujamiishaji wa kiduara.Uzuri kwa waafrika upo katika umbo la kiduara kwani huamini kuwa kila kituchenye umbo la duara kina uzuri ndani yake. Hii inatokana na mwafrikaanapoamini kuwa maisha yapo katika mzuknguko wa kiduara kwamba kuna; kuzaliwa,kuota meno, kuoa au kuolewa, uzee, kufariki, mizimu na kuzaliwa tena upya.Mwafrika anaamini kuwa mtu akifa huzaliwa tena upya na watu huwatokea kwa surambalimbali hii inaonenaka katika kurasa nyingi za riwaya hii ya BABUALIPOFUFUKA pale ambapo babu aliyefariki zamani humtokea K kwa sura ya derevawake lakini pia K naye anapofariki huwatokea akina Binti Kidawa pembezoni mwabarabara akiwa ameokota mkate kwenye pipa la taka. Mwandishi anasema; “Kidawa,aliita.

Wewe nani unayeniita mimi? Kidawa alikuwa kamtolea macho K. mimi babayako. Hnn! laiti ungelijua unasema nini … Ningelikuwa najua wewe ni baba yangu,ningelikuua hapahapa … lakini n’najua baba yangu ameshakufa … na wala sijutii.”Uk.166-167 Anendelea ukurasa wa 168; “N’tajaributena kujibidiisha na kujigeuza hai. Nitajaribu tena kukutafuteni nizungumzena’nyi. Ni muhimu. Leo ni siku ya mwanzo sikuwa na nguvu za kubaki hai mudamrefu.

“Hiiinadhihirisha kiasi gani mwafrika amekuwa na Imani ya kuwa maisha yake yapokatika uduara kwamba akifa huzaliwa tena na kuwa hai kwa upande mwigine.Mwafrika hasahau jadi yake au imaniyake ya awali. Nikwamba hata kama mtu wa kiafrikaameshika imani yake au kukaa mbali na jamii ama jadi yake ni lazima siku mojaatarejea kwao au atarudi nyumbani kwao kutokana na sababu mbalimbali.

           Mfano katika riwaya hii ya BABUALIPOFUFUKA mwandishi anasema; “kusemakweli, K asingeweza kupotewa na kijiji chao; hata ingekuwaje! Wenye kujuaukweli wameshasema mtu kwao! Siuwongo.” Uk.105 Anadhihirisha wazi jinsi mwafrika alivyojijengea utamaduditoka zamani kukumbuka nyumbani alikozaliwa kwa sababu mbalimbali kama vilematatizo, kifo ama hata kuhitaji Baraka za wazee ama za ukoo.Ulimwengu wenye nyuga kuu tatu. Waafrikawanaamini kuwa ulimwengu umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni ardhini auduniani ambako huishi watu na mizimu, kuzimu ambako inaishi mizimu au wahengawaliokwisha kufariki na juu mbinguni ambako anaishi Mungu na miungu waafrikawanaamini kuwa kuna Mungu mkuu na miungu wadogowadogo. Ili kumfikia Mungu mkuukuna darajia mbalimbali ambazo lazima mtu apitie ambazo nimtu-wazee-mizimu-miungu-mungu. Mwandishi wa riwaya hii ya BABU ALIPOFUFUKAanadhihirisha hili pindi anapomuonesha mhusika K ambaye anafariki na kwendadunia nyingine iitwayo jehanamu (kuzimu).

K anasema; “Pu!Na fyoko; alifyokonyoka kutoka kitundu kidogo cha njia ya mchwa kutoka chini yaardhi. Akajikuta kwenye Jahanamu. Dunia ngeni ya kitisho na kuogofya. Yakukatisha tamaa. Akajikuta kasimama kwa hofu. Akagwaya kasawijika uso na mwiliukimtetema.

Akatupa jicho kulia, jicho kushoto. Tena nyuma na mbele. Mazingiramahame.”Hivyobasi tunaona kwamba waafrika wanaamini kuwa mtu akizaliwa anaishi katika dunia,akifa anaenda kuzimu au jahanamu na badaye baada ya kuchunguzwa dhambi zakeanaweza kuhamia sehemu ambayo ni Mbinguni ambako yuko Mungu mkuu.Itikadi ya kani. Falsafaya kiafrika inaamini kuwa kuna kani (nguvu) katika vitu, kauli, heshima,ushujaa, miiko, kiapo na laana.

Katika riwaya ya BABU ALIPOFUFUKA Mwandishianathibitisha jambo hili katika ukurasa wa 143 -144 mwandishi anaonesha nguvuya kiapo pale kiongozi wa wakati akimwambia K anasema; “kwambaitabidi ule kiapo. Je, unajua maana ya kiapo cha jadi ambacho wamasai nawakamba wanakitumia mpaka leo? “Sijui chochote kuhusu ushirikina.” “Nitakwambiahivi basi … tutatambika tutakuapisha kiapo cha kimasai na kikamba; kiapo chaKithitu au Ndundu.”Hivyobasi, jamii mbalimbali za kiafrika zinaamini katika nguvu ya kiapo, miiko,laana, heshima na kadhalika. kwa mfano jamii za kanda ya ziwa hususani wakuryawanaamini katika nguvu ya kiapo kwa mfano, mtu na rafiki yake wa amini wakilakiapo siyo vizuri kwenda kinyume na kiapo hicho mfano mtu kutembea na mke warafiki yake au kumuibia.

Endapo atavunja kiapo hicho na miiko yao jambo bayalaweza kumtokea kutokana na nguvu ya kiapo chao.Uyakinifu wa kipragmatiki. Mwafrikaametawaliwa na mtazamo wa kujali maisha ya sasa kuliko ya jana na kesho naanajali vitendo kuliko nadharia. Katika riwaya hii ya BABU ALIPOFUFUKA mwandishianaonesha jinsi baadhi waafrika walivyosahau maisha waliyopitia na sasa wanamaisha mazuri hivyo hawakumbuki shida walizopitia.

Mfano K amesahau kabisakuhusu maisha yake ya awali kipindi yupo Kataa. Sasa hivi anajivinjari utajirihuko mjini amesahau kabisa kwamba kuna jana na kesho. Katika ukurasa wa 21mwandishi anasema; “sikuweza kuingia kwa sababuya farakano baina ya maisha yako yaliyokimbilia upande mmoja… umebadilikahukumbuki uipotoka”.Kuheshimu wahenga na mahoka kwa njiaya matambiko ambapo wahenga hukumbkwa kwa majina na kutambikiwa. Katikariwaya hii mwandishi anasema; “aliyekufaanaweza kufuffuka K. hasa hapa petu! Hapa penye maisha ya uhenga na uzuka,maisha ya kufa na kufufuka”. Kwa hiyo tunaona kiasi gani waafrikawanathamini na kuamini mizuka na wahenga katika maisha yao ya uhai na kifo.Wanaamini kuwa wahenga na mahoka ndio wenye uwezo wa kufikisha matatizo yao kwamungu na kuweza kutatuliwa kiurahisi.

Na pia wahenga wanaaminiwa kuwa ndiohutoa maadili mema na mwongozo wa maisha.Hivyobasi falsafa ya kiafrika inapaswa kutazamwa kwa upana kutokana na imani yake,mienendo yake, desturi, msingi na miendelezo inayolenga maisha yao kwa ujumla.Kuna haja ya kuendeleza falsafa ya kiafrika na kuacha kukumbatia falsafa zakigeni kwani ili tuweze kujikomboa kifikra tunapaswa kuzikomboa nafsi zetukwanza. Japo kuwa wataalamu wengine nje na Afrika wanasema hakuna falsafa yamwafrika au kama ipo basi ni falsafa isiyokuwa na maendeleo.

Hivyo ni lazimatupinge mawazo hayo na kuendeleza imani, mienendo na mitazamo yetu katika jamiizetu za kiafrika ili kuondokana naa fikra za kitumwa kwa sababu hata historiainaeleza kuwa kufikia karne ya 15 Afrika na Ulaya walikuwa katika usawa wakimaendeleo, kitekinolojia na historia ya falsafa yake. Mfano ulaya kunawanafalsafa kama Plato na Aristotle wanathibitisha jambo hili kwani waliwahikusoma falsafa ya Afrika. Tunaelezwa kuwa Misri na Timbuktu ilikuwa ndiyokitovu cha falsafa.

    MAREJELEO http://www.jamiiforums.com/threads/umuhimu_wa_falsafayakiafrikaHanson,B. (2004). Takadini. Methews: Book Stone and Stationery.

Mbiti,J. (1990). African Religion and Philosophy. New York: Praeger publisher.Mohamed,S. A. (2001). Babu Alipofufuka.

Nairobi, Kenya: English Press ltd.Mung’ong’o,C. (1977). Mirathi ya Hatari. Dar es salaam: Tanzania mPublisher House.Temples, P.

(1959). The Bantu Philosophy. Paris:Presence Africaine.   TUKI.(2004).

Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: Taasisi ya Uchunguziwa Kiswahili.Wamitila,W.

(2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: FocusPublications. 

Post Author: admin

x

Hi!
I'm Eric!

Would you like to get a custom essay? How about receiving a customized one?

Check it out